| Zaidi ya vikundi na wasanii
mia moja hamsin wameshiriki katika moja ya matamasha yaliyopita
ya Sauti za Busara na baadhi yao ni Jose Chameleone, Juma
Nature & Wanaume family, Saida Karoli, Didier Awadi & Phat
4 (Senegal), Mchinga Generation, Eric Wainaina (Kenya), Ghorwane
(Mozambique), The Shrine Synchrosystem (Uingereza),
Taffetas (Uswisi), Atongo Zimba (Ghana), Ellika & Solo,
African Revolution Band, El Tanbura (Misri), Seiyun Popular
Arts (Yemen), Culture Musical Club, Chibite na wengineo wengi.
Baadhi ya wasanii wa Afrika ya Mashariki
kama Afrikali Band, Oya Theatre, Zemkala, Jagwa music, X
Plastaz, Maulid ya Hom, Sina Chuki Kidumbak na wengineo wameanza
kupata mialiko ya kushiriki matamasha nje ya nchi baada ya
kuonekana katika tamasha la Sauti za Busara.
Je unataka kushiriki?
Kwa wasanii wanaotaka kushiriki katika tamasha lijalo la
2008, unatakiwa kutuma maombi yako kabla ya mwisho wa
mwezi wa Agosti. Tuma maombi yako kwa njia ya barua
pepe (email) au barua ya kawaida kwa ofisi ya Busara
Promotions (Anuani hapo chini). Maombi yaambatane na nakala
za kazi yako ya hivi Karibuni (CD, Kanda za kaseti na/au
video). Picha pamoja na maelezo ya kina ya msanii au kikundi,
na pia kama una kumbukumbu za maelezo kutoka katika vyombo
vya habari juu yako tafadhali ambatanisha pia.
Kwa wasanii wanaochaguliwa kushiriki
katika tamasha la Sauti za Busara, gharama zao za usafiri,
malazi, chakula na malipo ya onyesho zitalipwa na waandaaji
(Busara Promotions). Wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki
watatakiwa kujilipia wenyewe gharama za usafiri.
|
Maeneo yenye alama ya * ni lazima
NB This form is also AVAILABLE IN
ENGLISH. Please choose BEFORE starting to fill in
the details.
Fomu hii inapatikana KWA KIINGEREZA
PIA. Tafadhali chagua kabla ya kuanza kuijaza.
|